GET /api/v0.1/hansard/entries/286473/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 286473,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/286473/?format=api",
    "text_counter": 373,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Ninashukuru kwa nafasi nimepata ili niweze kuchangia Hotuba ya Rais ambayo alitoa kwa taifa nzima kupitia Bunge letu na vyumba vya habari. Hotuba ya Rais vile inavyozungumziwa na wenzangu imekuwa na mambo mazito sana. Hasa nikisikiza Rais kwanza ninamshukuru kwa kuzungumzia kuhusu umoja wa Wakenya, kutaka kuwaleta Wakenya pamoja na vile vile kuongea hata juu ya siasa ambazo zinafuata na ambazo zinakuja. Rais alizungumza kuhusu maendeleo ya nchi na hasa mambo yanayomuhusu mwananchi wa kawaida. Katika Hotuba ya Rais, nilishindwa kupata na kufuatilia kuelewa kwamba mwananchi wa kawaida kwa siku zijazo atasaidika namna gani. Maendeleo makubwa yamefika mashinani na kuweza kuonekana na wananchi. Barabara na vyumba vikubwa vinajengwa. Pia, kuna mambo mengine ambayo yanafanywa. Lakini jambo la muhimu ni kwamba ukiangalia kazi ambayo Serikali inafanya na mahali ambapo mwananchi wa kawaida yuko ni dhairi kwamba mwananchi wa kawaida hajaweza kujihisi na kujisikia kwamba kweli Serikali inafanya kazi. Ni kwa sababu gani? Tunapojenga barabara, ndio, tunajenga barabara za juu na kutumia pesa nyingi; tunajenga barabara za kimataifa lakini wananchi wanaotumia hizo barabara, kati ya milioni 40 ni kama asili mia tano tu wanaoweza kuelewa chanzo cha barabara. Bw. Naibu Spika wa Muda, sehemu ninayowakilisha Bungeni inapakana na Nairobi. Kutoka hapa kwenda eneo langu la Bunge ni kilomita 65 tu, lakini ninakuahidi kwamba kati ya wananchi ninaowakilisha, watu takribani 275,000, ni wananchi asilimia tano tu wameweza kutembea katika barabara za lami na kuja Nairobi. Umaskini umekumba taifa nzima na haswa mwananchi wa kawaida kule chini; inakuwa ni vigumu kwake kuamua kuja Nairobi kufanya jambo kwa sababu hata pesa za kulipia nauli ya kumleta hapa hana. Tunapozungumuzia mambo ya maendeleo na kiwango cha maendeleo utaona kwamba mwananchi wa kawaida bado hana maji. Mwananchi wa kawaida bado hana matibabu ya kumfaa. Mwananchi wa kawaida hana mshahara wa kumwezesha hata kuishi kwa siku moja, wacha mambo mengi. Ninazungumuza kuhusu madawa; tumejenga mahosipitali na CDF imetusaidia kujenga sehemu za matibabu, lakini ni dhahiri kwamba hata wewe mwakilishi yeyote ambaye yuko hapa anajua kwamba mbali na kuwa tunajenga sehemu hizo na maendeleo hayo yote tunafanya ili wananchi watibiwe, tunakosa mambo mengi sana ya kuweza kutoa matibabu. Hivi sasa ninashangaa tunapozungumuzia mambo ya bima na National Hospital Insurance Fund (NHIF) nimeshindwa kuelewa--- Hata katibu wa chama cha wafanyikazi anapinga ada inayotolewa na mtu ambaye anapata mshahara wa juui. Tunafahamu kwamba kanuni ya ulipaji wa kodi ni kwamba nyingi unazopata, nyingi unastahili kutowa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama mtu anapata Kshs500,000, kwa nini ada yake ya bima ya hosipitali iwe sawa na ya yule anayepata mshahara wa Kshs7,500? Desturi ya nchi inayoendelea ni kwamba walio na uwezo wanatoa zaidi ili kuwezesha kuwamudu walio na mapato ya chini. Ninamaanisha nini? Ninamaanisha kwamba hivi sasa kama malipo yangu ya bima ni Kshs3,000 mimi sitashindwa kulipa. Mshahara ninaopata Bungeni na katika kampuni yangu, hata kama nitatozwa ada mara mbili, hii pesa itasaidia mwananchi kule Ugenya ambaye hana kazi na hosipitali itakuwa na madawa. Sasa imekuwa ni kasheshe na siasa. Tunasema malipo ya bima ya matibabu yawe ni sawa. Kwa nini Katibu wa Kudumu serikalini, ambaye mshahara wake ni Kshs800,000 alipe Kshs250 huku mwananchi ambaye ni mwalimu na ana Kshs6,000 vile vile analipa Kshs200? Wakenya tumekuwa watu wa kuingiza siasa pahali siasa hazitakiwi. Mimi ninataka kusema hivi, mwenye kupata nyingi atoe nyingi ndipo mwenye kupata kidogo aweze kufaidika. Tukienda hivyo tutajenga na tutakuwa na taifa lenye msingi imara na lenye nguvu. Kwa hivyo katibu wa vyama vya wafanyikazi aelewe kwamba mbali na yeye kuwa anataka kura za wafanyikazi anaumiza watu, wakiwa ni pamoja na hata dada yake ambaye hafanyi kazi. Hii ni kwa sababu ile ada inatolewa na yule mtu ana nyingi itasimamia matibabu ya yule ambaye hafanyi kazi. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunaona watu wenye akili zao wakienda kortini kusimamisha malipo ya ada hiyo na huku mtu ana mshahara. Wanaopata pesa nyingi wanalipiwa hata matibatu na makampuni na serikali. Mimi mwenyewe nina bima ya Kshs10 million; hii ni yangu, watoto wangu na mke wangu. Mwananchi aliyenipigia kura hana bima hata ya Kshs200 ya kumwezesha kutibiwa. Sisi hushangilia na kwenda kufanya mikutano na kuzungumuzia mambo ambayo yatatuwezesha kupata kura. Hata mbele ya Mwenyezi Mungu hakuna haki aina hiyo. Ni dhahiri kwamba kama malipo ni mengi ni lazima utoe mengi ndiyo umsaidie aliye chini. Jambo lingine ambalo nataka kuliguzia ni kwamba tukisema leo maendeleo yako, na mwananchi wa kawaida katika taifa letu ameajiriwa na kampuni ya kibinafsi ama na serikali, bado anaumia. Ninazungumuza kwa kuwa ninaujua ukweli na nimeweza kushuhudia mambo haya. Bw. Naibu Spika wa Muda, Rais alipozungumuza hapa alisema tukae pamoja na tuungane tujenge taifa lenye nguvu na msingi mmoja. Lakini hilo halitaweza kupatikana kama mwananchi wa kawaida kama mwalimu hana mshahara. Mwalimu wa leo mshahara wake ni Kshs7,500. Huyu ni mtu aliye na watoto na anataka mtoto wake asome amalize shule ya msingi, aende shule ya upili na vile vile aende kiwango cha juu cha elimu, na huku tunasema kwamba tuna maendeleo, na tunajenga barabara zinazopita magari manane kwa wakati mmoja. Watu tunaojengea barabara hawawezi kujimudu; itakuwaje wewe unajenga nyumba ya vyumba 50 na watoto wako ni wawili na unajua pesa ya chakula na mavazi hakuna? Mbali na kuwa tunajenga na tunataka kuona nchi inaendelea, tuzingatie maisha ya watu wa sasa. Hatufai kuongoza wanyonge ambao hali yao ya afya ni mbaya na watakufa kesho na umasikini. Nani atatumia maendeleo tunayoyaweka? Tunajengea nani hizi nyumba kubwa kama wananchi hawatakuwepo kuweza kuzitumia. Tunaweka msingi wa mwananchi mwenye afya duni ambaye hana akili na hana nguvu ya kufanya kazi. Haya maendeleo tunaletea nani? Tunaletea watakao kuwa na nguvu ambao ni wachache, maana ndio watakaobaki katika taifa hili wale wanyonge watakapokuwa wameenda kabisa na hawaonekani. Ni lazima tuzingatie na kuona kwamba tunaweka misingi ambayo inamwezesha mwananchi wa kawaida kuinuka, ndipo aweze kufurahia maendeleo katika taifa letu. Ninaunga mkono."
}