GET /api/v0.1/hansard/entries/288702/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 288702,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/288702/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bi Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Swali hili linalenga maeneo mengine nchini ambapo mabwawa yake yamejaa mchanga na hayawezi kutumiwa katika kuvuna maji wakati huu wa masika. Wakati huu mvua ni nyingi sana na inasababisha vifo vya watu na wanyama wengi. Pia inasababisha harasa kubwa ya mali ya wananchi wa taifa hili. Ni mikakati gani mwafaka Wizara hii imeweka ili kuzuia hasara inayosababishwa na mvua katika maeneo mbalimbali nchini? Tumeshuhudia nyumba za watu na majengo mengine yakibomolewa na mafuriko ya maji. Mifugo na watu wengi wamepoteza maisha yao. Miaka nenda, miaka rudi, tunashuhudia mafuriko na baada ya miezi miwili ukame unaingia. Pia ukame husababisha hasara kubwa kwa watu na mifugo. Watu wengi hupoteza maisha yao kwa sababu ya njaa na mifugo hufa kwa sababu ya ukame. Je, Serikali hii inafanya nini ili kuvuna maji wakati wa mvua ndio watu wetu wayatumie wakati wa kiangazi? Mwenyezi Mungu hutupa maji mengi lakini sisi hatufanyi lolote kuyavuna ili tuyatumie wakati wa ukame."
}