GET /api/v0.1/hansard/entries/289128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 289128,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/289128/?format=api",
"text_counter": 622,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tumepitia kwa mikono ya walimu, hatuwezi kukumbuka uchungu waliokuwa nao walipokuwa wakitufundisha mpaka tukafika hapa tulipo. Eti sasa mawazo ya Mkuu wa Sheria yanahitajika kusudi malipo ya shilingi 3.34 bilioni yalipwe, pesa ambazo zimeshawekwa na Bunge hili kulipwa walimu. Ninasema kwamba hizi hela zilipwe kwa hima bila kupoteza muda kwa sababu ziko ndani ya Bajeti. Zile zilizobakia, karibu Kshs15 billion ziangaliwe na kupendekezwa kulipwa katika mwaka mpya. Hata hivyo, sheria iliyopo, na ninataka kuwatia hawa walimu moyo ni kwamba sasa wao wanafanya biashara. Sheria ya sasa inasema kwamba hadi utakapolipwa marupurupu yako ya kustaafu wewe utahesabika kama mfanyakazi wa Serikali na unaendelea kulipwa mshahara wako na marupurupu yako. Hii ndio sheria tulipitisha katika Bunge hili. Hawa walimu, kuanzia mwaka wa 1997 hadi mwaka 2003, ni haki yao kama hawatalipwa waende kortini na kusema kwamba wao wanastahili kulipwa hizo siku zote ambazo wamekuwa hawajalipwa marupurupu yao ya kustaafu."
}