GET /api/v0.1/hansard/entries/289130/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 289130,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/289130/?format=api",
"text_counter": 624,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, ni vizuri. Ninakubaliana na korti kwa sababu ni haki yao. Lazima wanyonge wapewe haki yao. Iwapo jambo kama hilo haliwezi kutiliwa maanani, ni jambo la vurugu, aibu na la laana. Ninafikiri hata sasa Waziri wa Elimu aliye hapa sasa Hoja hii inasema kwamba Kshs3.34 bilioni zinangoja fikira ya Mkuu wa Sheria. Hawakutoa mawazo ya kukataa au kukubali. Ni fikira zake tu. Kwani kupata fikira kuna shida gani? Kuna shida gani kupata fikira za Mkuu was Sheria? Pata hizo fikira. Mawazo yake hayawezi kutufunga sisi kama Bunge. Uamuzi umepitishwa kwamba hizi hela zilipwe walimu. Sitaki kusema mengi ya ziada. Mimi ninaunga mkono Hoja hii. Ninampongeza mwalimu John Pesa kwa kuwakumbuka hawa walimu, na kuleta Hoja hii katika Bunge. Ninaunga mkono kabisa Hoja hii. Jambo ni moja tu, walipwe."
}