GET /api/v0.1/hansard/entries/289935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 289935,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/289935/?format=api",
"text_counter": 391,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipatia fursa hii. Ningependa kuwapongeza watu waliokuwa wakishindania viti vya Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki. Pia, ninataka kuwapongeza Wabunge wenzangu kwa kazi nzuri tuliyofanya. Pia, kwa Wakenya, kuna funzo: Kwamba, Wabunge wakikaa pamoja hawakosani, na tusitoke nje kwenda kuwakosanisha watu wetu. Kwa hivyo ninataka kuwapongeza wale walioteuliwa kutuwakilisha katika Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki na kuwashauri kwamba wanakwenda kupeperusha bendera ya Kenya na kutufanyia kazi kama Wakenya. Jumuia ya Afrika Mashariki ni muhimu kwetu sote ambao tuko katika eneo la Afrika Mashariki. Ninataka kuwapongeza wale akina mama wanne waliopata vyeo hivyo leo na kuwahimiza kwamba wasisahau kwamba wao ni akina mama, na wao ni Wabunge; na wana haki ya kuipeperusha bendera yetu ya Kenya. Ahsante, Bw. Spika."
}