GET /api/v0.1/hansard/entries/290883/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 290883,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/290883/?format=api",
"text_counter": 398,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Shukrani, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninataka kuunga mkono Hoja hii. Kwanza, ningetaka kumshukuru mhe. Pesa kwa kuwasilisha Hoja hii hapa. Ningetaka kuwapongeza waalimu kutoka pembe zote za taifa letu kwa huduma bora ambayo wanatoa kwa taifa hili kwa kuwatunza watoto wetu na kuhakikisha kwamba sisi kama taifa tunaelekea kupata malengo yetu katika Idara ya Elimu. Ni swala la kufedhehesha sana jinsi ambavyo Serikali ya taifa hili inavyoshughulikia maswala ya watumishi wa umma kwa jumla, hasa watumishi wa umma ambao wemestaafu na ambao wamehudumia taifa hili na wakafikia muda wa kustaafu. Si waalimu peke yao, ukitazama Wakenya wengi waliostaafu baada ya kuhudumia taifa hili kwa njia sawasawa, utapata kwamba wengi wao wanaishi katika masaibu yasiyo kifani. Hii ni kwa sababu ya jinsi tunavyoshughulikia swala la malipo ya uzeeni. Kila mara, utakutana na Wakenya waliostaafu wakiwa na kilio kikuu kwa sababu ya shida ya malipo ya uzeeni na jinsi wanavyolipwa. Tunapolizungumzia swala hili la waalimu waliostaafu, nikielelezo na mfano wa jinsi ambavyo Serikali yetu haijashughulikia kikamilifu malipo ya uzeeni kwa wale ambao wamehudumia taifa hili na wakastaafu. Ukitazama kundi la waalimu ambalo tunalozungumzia, ni waalimu waliostaafu kati ya mwaka wa 1996 na 2003. Kundi la kwanza lilistaafu mwaka wa 1997, miaka 15 iliyopita. Tafakari swala la mwalimu aliyehuduma na akastaafu miaka 15 iliyopita. Mtoto aliyezaliwa mwaka wa1997, wakati huu pengine yuko katika Kidato cha Tatu na anaelekea kukamilisha masomo ya shule ya upili. Lakini mwalimu huyo, baada ya kuhudumia taifa hili kikamilifu, miaka 15 baada ya kustaafu, leo hii bado anakumbana na masaibu ya kutafuta malipo yake ya uzeeni. Kwa hivyo, hili ni swala la kufedhehesha na kuaibisha. Ni swala ambalo ninatarajia Serikali - na ninamwona ndugu yangu, mhe. Mwatela, kwa niaba ya Wizara ya Elimu yuko hapa - iombe msamaha itakapokuwa ikijibu Hoja hii. Kwanza, waalimu ambao tunazungumzia wanastahili kuombwa msamaha na Serikali kwa sababu bado wanatafuta marupurupu yao na malipo ya uzeeni miaka 15 baada ya kustaafu. Swali lingine la kutia wasiwasi ni kwamba Serikali hii imekuwa na mazoea kuwa ndio itimize lo lote, ni lazima isukumwe. Ni lazima kuwe na msukumo, maandamano na Mswada hapa Bungeni. Ni lazima kuwe na kilio ndio Serikali hii ichukue hatua au waalimu waajiriwe kazi. Tunajua hatuna waalimu wa kutosha. Lakini ili tuaajiri waalimu wa ziada, ni lazima Serikali isukumwe. Ni lazima chama kinachowakilisha maslahi ya waalimu, KNUT, kitoe ilani ya mgomo ndio Serikali isikize. Ili waalimu walipwe zaidi kama inavyostahili ni lazima kuwe na msukumo. Hivi juzi, waalimu 10,000 waliajiriwa kwa kandarasi na ikawa waajiriwe kwa utaratibu unaostahili. Ilibidi kuwe na msukumo hapa Bungeni na mgomo kule inje kupitia KNUT ndio Serikali ikasikiza kilio hicho na kuwaajiri waalimu hao. Tunapojadili Hoja hii, kuna tishio kuwa shule za umma zitafungwa Kenya nzima kwa sababu Serikali imezembea kutuma fedha za kufadhili mpango wa elimu ya bure katika shule za msingi na msaada katika shule za upili. Kwa sababu ya kuchelewa huko, kuna tishio kuwa shule zitafungwa katika pembe zote za taifa hili."
}