GET /api/v0.1/hansard/entries/290884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 290884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/290884/?format=api",
    "text_counter": 399,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Namwamba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 108,
        "legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
        "slug": "ababu-namwamba"
    },
    "content": "Nilishangazwa na Waziri wa Fedha akitangaza ya kwamba fedha hizo zimechelewa kwa sababu kuna jamaa fulani katika Serikali hii alisahau kutia fedha hizo kwenye makadirio ya pesa katika Bajeti ya muda tuliopitisha mwezi wa nne. Ni fedheha hiyo. Utasahau namna gani mpango huu wa elimu ya bure ulianzishwa na Serikali ya Mheshimiwa Rais Kibaki mwaka wa 2003? Kila mwaka tangu mwaka huo; 2003, 2004, 2005, 2006, 2007, 2008, 2009, 2010 na 2011 Serikali imeweka pesa hizo katika makadirio ya Bajeti. Itakuwaje leo utueleze ya kwamba ulisahau kukadiria fedha ambazo umezikadiria na ukazishugulikia kwa muda wa miaka kumi mfululizo? Kwa hivyo, hiki ni kielelezo cha Serikali ambayo kidogo imechanganyikiwa. Na hili swala la kwamba ni lazima Serikali hii isukumwe ndiposa itimize malengo fulani, ni swala ambalo lazima Serikali hii ilishugulikie kwa njia ya dharura."
}