GET /api/v0.1/hansard/entries/290885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 290885,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/290885/?format=api",
    "text_counter": 400,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Namwamba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 108,
        "legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
        "slug": "ababu-namwamba"
    },
    "content": "Nataka kuunga mkono Hoja hii kwa kusema kwamba fedha hizo si kiwango ambacho tutasema ya kwamba lazima tuende nchi za ugeni kukopa. Ni pesa ambazo tuna uwezo kama taifa kuzilipa. Hiyo ni kuonyesha kwamba Serikali hii haina nia ya kulipa fedha hizo na huo ndio wasiwasi wangu. Hata baada ya kuelewana na mkataba kutiwa sahihi, Serikali imejaribu kukwepa kulipa fedha hizo kupitia mahakamani. Na hata Serikali imefika hadi Mahakama Kuu kujaribu kuzuia malipo hayo ya Kshs17.6 bilioni. Ukilinganisha fedha hizo na fedha zinazofujwa; fedha zinazotumika kwa njia mbovu katika idara mbalimbali za Serikali, hauwezi hata kulinganisha. Ni fedha kidogo sana ukilinganisha na fedha zinazofujwa na Serikali. Safari za kila mara za mawaziri na maafisa wengine wa Serikali huku na kule, il hali, fedha hizo hazijalipwa ni aibu sana. Ninaamini kuna waalimu wengi waliostaafu na wameaga dunia. Nimesema kwamba kundi la kwanza lilistaafu miaka 15 iliyopita. Ninaamini kuna waalimu wengi waliostaafu ambao walipitia masaibu yasiyo kifani kabla ya kuaga dunia bila kuona malipo hayo. Familia zao zinaendelea kupata taabu. Kwa hivyo, swala hili ni swala la haki za kibanadamu. Ni haki ya Mkenya inayokandamizwa. Ni haki ambayo tumeiweka katika Katiba mpya ya taifa hili. Ninataka kusema ya kwamba tushughulikie swala hili kwa njia ya dharura. Na ikiwa ni kweli tuliweka Kshs3.34 bilioni katika Bajeti - makadirio ya Bajeti ya mwaka unaokamilika sasa hivi - ni nini kimezuia Serikali kulipa angalau shilingi hizo 3.34 bilioni ambazo tayari zimo kwenye Bajeti? Je, fedha hizo ziko wapi? Fedha za kufadhili mpango wa elimu ya bure ziko wapi? Waziri atakapojibu Hoja hii, aeleze taifa la Kenya hizo Kshs.3.34 bilioni zilizowekwa katika makadirio ya fedha katika Bajeti inayokamilika wakati huu, kabla hatujaenda katika Bajeti wa mwaka ujao, ziko wapi? Zimefanya kazi gani? Na kama ziko kwenye mfuko wa Serikali, mbona fedha hizo hazijalipwa?"
}