GET /api/v0.1/hansard/entries/291813/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 291813,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/291813/?format=api",
    "text_counter": 438,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kuulizwa na Serikali kujibu na kusema itatekeleza, inasikitisha wakati mwingine kwamba Serikali inatoa ahadi hapa Bungeni kwamba italitatua jambo hilo, lakini inachukua mwaka mzima na hakuna hatua ambayo Serikali imechukua. Kuna uhusiano kati ya kuuliza Swali na kutekelezwa na kuuliza Swali na kutojibiwa kwa wakati mwafaka. Tunataka kusema na kutenda. Kuna Kamati Tekelezi ya Bunge. Ni hatua gani ambayo Kamati hii inachukua kuhakikisha kwamba ahadi zinatimizwa? Kama taarifa iliombwa, ikatolewa na ikasemekana kwamba baada ya miezi sita hatua fulani itakuwa imechukuliwa na kama Swali limejibiwa na ikasemekana kwamba kwa majuma mawili jambo hilo litakuwa limetatuliwa, Kamati Tekelezi ya Bunge inachukua hatua gani kuhakikisha kwamba maswala haya yote yanafuatiliwa ili Taarifa na Maswali hapa Bungeni yasije yakaitwa, nikinukuu kwa lugha ya Kiingereza, public relations exercise kwa Wakenya? Tutakuwa tunahadaa Wakenya."
}