GET /api/v0.1/hansard/entries/291955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 291955,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/291955/?format=api",
    "text_counter": 580,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Thursday, 7th June, 2012(P) Mr. Namwamba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kumpongeza huyu Waziri Msaidizi kwa jinsi alivyoshugulikia swali hili na kutambua kwamba hili ni swala muhimu na ambalo limewakera Wakenya wengi katika sekta ya elimu. Ingawa tunashukuru kwamba suluhu imepatikana, na imepatikana kwa muda ufaao; kwa haraka sana, swala sugu ama swala nyeti ambalo linanikera mimi na ninaamini ni swala ambalo Wakenya wengi wangependa kusikia jibu kutoka kwa Waziri Msaidizi kwa niaba ya Serikali, ni kwamba, ni nini hasa kilitokea? Ni nini kilichosababisha fedha hizi kuchelewa kiwango kufikia kwamba imebidi kuwe na msukumo, vitisho na nia ya waalimu kugoma ndiposa Serikali ikachukua hatua hii ya kutafuta fedha hizi? Kwa nini Serikali imekuwa na mtindo kwamba kabla haijasukumwa, haiwezi kutenda jambo lolote na hasa kwa mambo yanayohusu elimu? Ni lazima kuwe na vitisho vya waalimu kugomo ndiposa Serikali ichukue hatua."
}