GET /api/v0.1/hansard/entries/292156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 292156,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/292156/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Machage",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": " Mhe. Spika, wakati huu wa majonzi, tunapoomboleza vifo vya rafiki zetu, kwa niaba yangu mwenyewe na jamii ya eneo la ubunge la Kuria, ningetaka kutoa rambirambi kwa jamii ya wote waliofiwa, hasa wale tulikuwa nao ndani ya Bunge. Hata hivyo, mmoja wa askari waliokufa, Bw. Murimi, anatoka kwetu nyumbani. Nataka, kwa njia ya kipekee, kutoa rambi rambi zangu kwa jamii yao. Mwezi uliopita, haijapita punde, tulimpoteza rubani aliyekuwa katika ndege iliyoanguka Mkoa wa Kaskazini Mashariki, ikiwa na wanajeshi watano. Rubani huyo alitoka katika eneo langu la ubunge. Na sasa tena, tumempoteza ofisa mwingine tena katika ajali ya helikopta. Kwetu sisi, afisa mwenye cheo cha serjeant ni mkubwa sana. Tuna wachache walio na cheo kama hicho. Kwa hivyo, tuna huzuni sisi Wakuria katika wakati huu. Ombi langu kwa Serikali ni kwamba hao waje walindwe hasa katika wakati huu wa matanga. Vile tutakaowatendea wenzetu Mawaziri, na hao pia wasije wakasahaulika eti wao ni kupewa jeneza tu na gari la kupeleka mwili nyumbani. Kuna mambo mengi ambayo jamii hizo zinahitaji. Hata zile za marubani pia zinahitaji msaada wetu. Kwa wakati huu, hatuna lingine ila kuwafariji na kumwambia Mola awabubujikie amani moyoni. Ahsante."
}