GET /api/v0.1/hansard/entries/292278/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 292278,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/292278/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Serikali ningependa kutoa risala za rambirambi kwa jamii ya marehemu Prof. George Saitoti, Bw. Orwa Ojode, marubani na askari waliokufa katika ajali ya ndege ya juzi. Bw. Spika, ajali hii ilikuwa pigo kubwa sana kwa taifa letu la Kenya, maana yake tumepoteza watu ambao kila mmoja ameongea hapa amesema walikuwa wazalendo; Prof. George Saitoti na Bw. Orwa Ojode walikuwa wazalendo. Bw. Spika ukitaka kujua mungwana ni nani, ni mtu kama Prof. Saitoti. Tunasema muungwana ni yule mtu amestaarabika na ustaarabu ni vitendo. Mtu huangaliwa kwa vitendo vyake, na Prof. Saitoti alikuwa mungwana, maana yake alikuwa hana adui na alikuwa ana heshimu watu. Alikuwa Makamu wa Rais kwa miaka 13 lakini alipokuwa Waziri, alikuwa chini yangu kama Waziri Mkuu na alinipatia heshima ya kutosha. Prof. Saitoti aliipenda kazi yake na aliifanya kwa ukakamavu bila chuki yoyote. Bw. Ojode vile vile, kama vile Wabunge wamesema, alikuwa ni mungwana tena alipenda kuwachekesha watu. Alikuwa ameichukua kazi yake kwa umuhimu zaidi. Kwa hivyo, kwa hao wawili, tumepoteza wazalendo. Wakati kama huu kunakuwa na huzuni nyingi na chuki. Ningependa kuwahimiza Wakenya wote, sote tuwe na subira. Kama vile Rais alivyosema jana, tunataka kuona kama tutafika kwenye kiini cha ajali hiyo ili ijulikane ni nini iliisababisha. Kwa hivyo, hakuna mtu angependa au atajaribu kuficha yale yamefanyika, lakini tuwache uchunguzi ufanywe na wataalamu. Tumesema kuwa tuna mahakama lakini pia tutaunda kamati ya wataalamu ambao watafanya uchunguzi ili kubaini ni kitu gani kilifanya hii ndege ianguke; ilikuwa ni makosa ya rubani, hali ya anga, hitilafu ya injini au ni kitu gani? Kwa hivyo, ikiwa tungeweza kusubiri wakati huu, tunaweza kuwafanyia wenzetu ambao wametuwacha vizuri zaidi. Ningesihi wenzetu wote tufanye hayo wakati huu. Nikimaliza, Prof. Saitoti alipoongea juzi kule Mombasa alihimiza kila Mbunge ambaye alikuwa anashiriki huko achangie kwa kuona kwamba uchaguzi unaokuja utakuwa wa uwazi bila fujo yoyote ili kudumisha amani. Sisi sote tunahitajika kujiepusha na siasa ambayo inaweza kuleta moto na vile vile kuleta chuki baina ya makabila yote ya Kenya. Tuungane pamoja kama Wakenya ili tuweze kukumbuka wenzetu waliotuwacha na kufanya vitendo ambavyo wao wenyewe wangependa tuwafanyie. Vile vile, tunaomboleza wale waliokufa nao; marubani na askari kwa sababu wote ni Wakenya. Kwa hivyo, tumesema Serikali itagharamia mazishi ya hao watu wote na kuangalia jamii zao ili wasipate athari yoyote baada ya kuzikwa kwa wenzao waliotuwacha. Kwa hayo machache, ninasema Mungu aweke nyoyo zao mahali pema peponi."
}