GET /api/v0.1/hansard/entries/29236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 29236,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/29236/?format=api",
"text_counter": 950,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Mswada huu. Ghadhabu ya Wabunge hapa inatokana na mambo ambayo yametendeka. Kwa mfano, nilipeleka ripoti kwa Kitengo cha kupambana na Ufisadi na nikasema kuwa pesa fulani zilitumiwa vibaya kwa kununua shamba. Maofisa walitumwa katika sehemu yangu ya uwakilishi Bunge na wakafanya uchunguzi lakini kwa sababu ilikuwa haihusu Mbunge, ripoti hiyo iliwekwa kando na mpaka leo, sijapata jawabu. Katika nchi hii, kazi yetu ni kutengeneza tume baada ya nyingine. Tunaajiri askari baada ya mwingine na mwishowe, tunabaki na askari ambao hawafanyi kazi. Pesa nyingi zimeibiwa katika taifa letu na tangu tuunde kitengo cha kupambana na ufisadi, hatujasikia hizi pesa zikitajwa hata siku moja. Tunasikia kuwa Mbunge fulani ambaye ameandika cheti cha Kshs50,000 au Kshs20,000 ndiye anayefuatwa lakini walioiba pesa ambazo zimeangamiza na kuhujumu uchumi wa nchi hii wako huru na wanatembea na kufanya wanavyotaka. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumesikia mambo ya Triton. Baada ya kuweka watu ambao tuliweka afisini na kumlaumu Ringera kwamba hafanyi kazi na kubadilisha askari huyo na kuleta mwingine, aliyeenda pale hakupatwa na akili hata kidogo ya kusema kwamba pesa zimepotea kupitia Triton na kuwapatia Wakenya ushahidi kuonyesha anafanya kazi. Kimya, kimya! Jana, mtu aliyewekwa katika kitengo cha kupambana na ufisadi, mwili wake unazungumza kwa mafumbo akisema kwamba: “Mimi sungura mjanja, nimepata habari kwamba nitahongwa, nikakimbia nikajificha na nikaweka vifaa vya habari kumnasa anayekuja kunihonga”. Ni nani ambaye anastahili kumwambia anayemhonga kwamba hafanyi kazi namna hiyo? Angemwambia: “Wewe nenda nyumbani, tutafanya uchunguzi na kama hauhusiki, tutakuwachilia”. Kwa nini, kwanza, alikubali na yeye ndiye mtu anayefaa kukamata wafisadi? Anakubali pesa ziletwe na akijua zinaletwa, anaruka na kuanza kucheza kwenye vyombo vya habari. Hatutaki mchezo wa paka na panya katika taifa letu. Tunataka watu wakipewa kazi wanaifanya kwa bidii na kutoa uamuzi unaotakiwa na Wakenya. Watu wa Kangundo walitenga ekari 1,600 walipokuwa wakigawa shamba lao na wakasema kuwa kwa sababu wako karibu na Nairobi, itakuwa ni ya matumizi yao ya baadaye. Hivi leo, kuna kampuni zaidi ya mbili ambazo zimepewa barua za kumiliki shamba hilo kwa miaka 93. Nimeipeleka ripoti hiyo kwa Waziri wa Ardhi na anaangalia. Cha ajabu ni kwamba, mbali na kuwa hiyo ripoti nimepeleka katika kitengo cha kupambana na ufisadi, sijasikia jambo lo lote. Mimi ninalipa kodi ambayo inatumiwa kulipa watu ambao hawana kazi ya kufanya. Waziri anataka kutuambia kuwa hiki kijikaratasi kitafanya kazi? Tutaupitisha Mswada huu, lakini ningetaka Waziri arudi nyuma na atafute nguvu za kuuma. Hakuna meno ya kuuma kwa sasa katika kitabu hiki."
}