GET /api/v0.1/hansard/entries/296974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 296974,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/296974/?format=api",
"text_counter": 16,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Yakub",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 378,
"legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
"slug": "sheikh-dor"
},
"content": "Bw. Spika, asante na nitafanya haraka. Kuna barua ambayo imetoka kwa wakili wa jamii ya Wasiu ya kutaka Mkuu wa Wilaya wa Lamu Mashariki aketi pamoja na kamati ya Bw. Omar Sabur kuanzia 5/08/2012. Hilo halijafanyika. Pia kuna barua iliyotoka kwa wakili na iliyokwenda kwa Director of Physical Planning and Survey, Lamu. Pia, kikao hicho hajifanyika. Mwisho ni kwamba ni masikitiko ya kwamba kila Wasiu wakienda kwa ofisi ya ardhi, Lamu, hawaonyeshwi ramani na majina ya watu waliopewa stakabadhi ya kumiliki mashamba haya. Nafikiri jambo hilo si haki. Kila Mkenya ana haki ya kuomba stakabadhi anazotaka kutoka ofisi yoyote ya Serikali. Naweka hizi barua mbili za wakili kwenye Meza"
}