GET /api/v0.1/hansard/entries/29940/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 29940,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/29940/?format=api",
    "text_counter": 689,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Godhana",
    "speaker_title": "The Assistant Minster for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 23,
        "legal_name": "Dhadho Gaddae Godhana",
        "slug": "dhadho-godhana"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nataka kuunga mkono kwa dhati Hoja hii ya kuongeza muda kwa Tume hii. Sote tunajua malengo na madhumuni ya kuunda Tume hii ni kwa sababu ya kwamba tunataka kuhakikisha ya kwamba amani imepatikana hapa nchini. Tume hii inaweza kuchangia pakubwa katika kuleta amani na umoja wa Wakenya. Bila Tume hii itakuwa vigumu kwa sisi kutekeleza mipango yetu ya maendeleo. Kwa hivyo, ni muhimu ya kwamba Wabunge wenzangu waweze kuunga mkono Hoja hii kama vile wenzangu walivyosema. Bila kupoteza wakati mwingi, ninawasihi waheshimiwa Wabunge kuunga mkono Hoja ili Tume hii ipate muda zaidi wa kufanya kazi yake."
}