GET /api/v0.1/hansard/entries/300604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 300604,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/300604/?format=api",
"text_counter": 739,
"type": "speech",
"speaker_name": "75 Thursday, 28th June, 2012(P) Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi Naibu Mwenyekiti wa muda, naomba nichukuwe nafasi hii kusema kwamba kazi ambayo imefanywa na ndungu zangu hapa inaridhisha. Tusingefika hapo ikiwa Wizara ya Fedha isingekuwa na heshima kwa kamati za Bunge. Kwa maoni yangu, kama hundi hii ingeletwa awali iangaliwe kwa utaratibu na ichambuliwe ikizingatiwa kuwa Katiba imegeuka, huu mjadala haungefika hapa ulipofikia. Kama tunavyokumbuka ilikuwa ni Wizara ya Fedha--- Baada ya Bunge kukubaliana kwamba makadirio yangekuwa hivi na hivi wameenda wakachapisha Mswada wao ambao ulikuwa tofauti kabisa na yale makadirio ambayo yalikubaliwa na Bunge. Ni nini Wizara ya Fedha inaficha? Lazima iwe na uwazi. Natumaini kwamba Waziri, ijapokuwa wewe bado ni mwanamwali na ubishi unao, sasa umekomaa na umeshika ukakamavu, na kuwa utatenda kazi kulingana na Katiba mpya. Yale yaliyokuwa yakitendwa na Wizara ya Fedha ya kuona kuwa katika kutayarisha makadirio ya pesa ni wao wenyewe wana utaalamu, ufasaha, na sifa zote za kuleta makadirio ya pesa hapa, hayo yaishe. Naomba ushikane na kamati za Bunge. Wizara ikishikana na kamati za Bunge, angalia ile kazi imefanywa. Angalia hivi vipengele vitatu tumevikamilisha. Ule utata ambao ulikuwako sasa umeisha. Kwa hayo mengi naomba tu nikome hapo."
}