GET /api/v0.1/hansard/entries/301526/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 301526,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/301526/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Ochieng",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2955,
        "legal_name": "David Ouma Ochieng'",
        "slug": "david-ouma-ochieng"
    },
    "content": "Hoja ya nidhamu Bwana Naibu Spika. Tunashangaa sana kuona Waziri wa Kawi akihepa kuja hapa kulijibu Swali linalohusu Wizara yake. Sehemu ya Bura iko katika Mkoa wa Pwani. Huko ndiko tuna mambo ya MRC ambao wanasema kwamba wamekanyagiwa katika mambo ya maendeleo kwa miaka mingi. Hii ndio sababu wanateta. Kuteta kwao kutamalizwa vipi kama Waziri hawezi kuja hapa kutuambia ni lini atapeleka stima kule Bura? Ni lazima uhakikishe kuwa Waziri huyu amepewa siku 14 kupeleka umeme katika sehemu hiyo ili tusiwe na vikundi kama MRC vikiteta na kusema vimekanyagiwa maendeleo kwa miaka mingi."
}