GET /api/v0.1/hansard/entries/301532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 301532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/301532/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Ethuro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 158,
        "legal_name": "Ekwee David Ethuro",
        "slug": "ekwee-ethuro"
    },
    "content": "Kwa Hoja ya Nidhamu, Bw. Naibu Spika. Wakati tulipata likizo ya mwezi moja kwenda nyumbani, hiyo Hoja ililetwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni ambaye ni Makamu wa Rais na Mawaziri wenyewe wakaunga mkono, nasi pia tukakubali. Waliomba nafasi ya kuenda kutengeneza kazi ili wakati tutarejea katika Bunge hili watakuwa na majibu kwa Maswali. Hii ni siku ya pili tangu turejee na unaona kwamba Mawaziri walienda kulala badala ya kuenda kurekebisha kazi. Kwa hivyo, baadala ya Mhe. Obure, rafiki yangu, kuja kumtetea mwenzake, angekuja kujibu hilo Swali au angemtafuta. Ama atuambie ni kwa nini Mhe. Nuh anataka nuru kwa mambo ya Bura na Waziri huyu hampatii nuru Mhe. Nuh."
}