GET /api/v0.1/hansard/entries/302180/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 302180,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/302180/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Magerer",
"speaker_title": "Waziri Msaidizi wa Kawi",
"speaker": {
"id": 51,
"legal_name": "Magerer Kiprono Langat",
"slug": "magerer-langat"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. (a) Halmashauri ya usambazaji umeme katika sehemu za mashinani za nchi yetu ya Kenya ilianza kusambaza umeme katika soko la Bura mnamo 2009/2010 wa makadirio na matumizi ya pesa za Serikali. (b) Wakati ambapo laini ya kusambaza umeme ilikamilishwa mnano 24 Novemba mwaka uliopita na ikafunguliwa rasmi na Mhe. Makamu wa Rais, iligunduliwa baadaye kwamba laini hiyo ilikuwa na shida fulani. Kutoka siku hiyo, soko la Bura na sehemu nyingine hazijapata umeme kwa njia ifaayo. Nina furaha kuripoti kwamba kufikia tarehe 6 Juni 2012, hitilafu hiyo ilirekebishwa na sasa soko la Bura na sehemu nyingine zilizo karibu na Mji wa Bura zimepata umeme."
}