GET /api/v0.1/hansard/entries/302191/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 302191,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/302191/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Magerer",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 51,
"legal_name": "Magerer Kiprono Langat",
"slug": "magerer-langat"
},
"content": "Bwana Naibu Spika wa Muda, ninajua kwamba Mheshimiwa Duale hutatizwa na Kiswahili lakini lazima nimueleze. Ndugu yangu, tulia nikueleze kwa sababu umeuliza swali na ninataka nijibu. Wacha atulie ili nimpe jibu halafu aulize swali lingine. Nimesema mambo ambayo hayajafanyika hadi sasa. Mheshimiwa Dkt. Nuh, ambaye ni rafiki yangu, ameyaleta mbele yangu. Kwa hivyo, ninatoa hakikisho kwamba wiki ijayo, nitatembelea eneo hilo ili kuona shida iko wapi kama hatutakuwa tumerudisha nguvu za umeme."
}