GET /api/v0.1/hansard/entries/302553/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 302553,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/302553/?format=api",
    "text_counter": 532,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante Bi Naibu Spika wa Muda. Yangu yatakuwa machache sana. Ninaishukuru Kamati iliyoleta Hoja hii hapa na kazi iliyofanya ambayo ni ya maana sana huku nikizingatia kwamba Wakenya wanatuangalia na kusikiliza tunayoyazungumza kuhusu wale walioadhirika, wana shida na wanaishi nje. Ni aibu sana kuona sisi viongozi ambao tunategemewa katika taifa letu tukiwakosea wananchi wetu. Tulizunguka taifa nzima, tukawaitisha wananchi kura na wakaandamana katika mlolongo nyuma ya visanduku vya kupigia kura na wakatupa uwezo ili tuwaongoze. Tangu wakati huo, tumeishi maisha mazuri. Wenzetu wote, baada ya kupigiwa kura na wananchi ambao hawana tumaini lolote tumeishi maisha mazuri. Tunapata chochote tunachotaka, tunalindwa na Serikali na walioadhirika bado wako nje, wananyeshewa na wanalia. Kama kweli mwananchi wa kawaida hawezi kumlilia kiongozi aliyemchagua na amsaidie, basi taifa hili linaelekea wapi na matumaini ya watu hawa ni nini? Wanaweza kuenda wapi na wanaweza kumlilia nani? Tunajua Bajeti ilisomwa ina pesa ya kuwaangalia walioadhirika na kuwapa masha. Katiba yetu mpya tuliyoipitisha inazungumza wazi kwamba ni lazima kila mwananchi wa taifa hili awe na sehemu ya kuishi na kukaa lakini tunapozungumza sasa, kuna wananchi wanaostahili makao na kuna wananchi ambao hawastahili kuishi ila tu kulia siku zote."
}