GET /api/v0.1/hansard/entries/302557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 302557,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/302557/?format=api",
"text_counter": 536,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ni Kenya tu ambapo mambo ya kiajabu yanatokea. Juzi tumesikia na kusoma kupitia vyombo vya habari kwamba mwaka uliopita Serikali yetu ilirudisha kitita cha Kshs183 bilioni ambazo hazikutumika. Kama ni kweli pesa hizi zipo na zimerudishwa katika Serikali kuu na bado haijaingia katika mgawo wa matumizi ya Serikali ya mwaka huu, kwa nini hii pesa isipewe Waziri aliye hapa ili aende anunua mashamba ambayo yako ili awape wananchi waishi? Tunapozungumza tunawashangaza Wakenya kwa sababu katika makadilio ya Bunge tunatakiwa kupata marupurupu tutakapoenda nyumbani. Pesa hizi zinatufaaa kweli kama wananchi wako barabarani wakilia, kukasirika na kutuombea mabaya? Mtu na watoto wake wako nje na kuna Serikali ambayo ina askari, pingu na bunduki na vyombo vya kutia wahalifu ndani na hakuna kitu kilichofanyika na bado tunaongea! Sisi tunategemea kuenda kupiga kura na kuongea barabarani kuhusu amani ili Wakenya wasikie, tumekuwa wahubiri wa usiki ambao wanahubiri neno ambalo wao wenyewe hawaliamini. Tunategemea mtu ambaye yuko nje na watoto wake, mtu ambaye alitoa jasho kununua shamba lake na ambaye alipigwa na watu wengine atupigie kura? Kwani Kenya ina viwango vingapi vya wananchi? Hii ni Kenya ya wale walio juu au ni Kenya iliyo na usawa wa kila mwananchi? Kama ni ya usawa wa kila mwananchi, inakuwaje tunapanga kujenga mabarabara makubwa ambayo magari ya wakubwa yatapita? Hawa watu wanaingia kuwanyanyasa wananchi wadogo wanaoishi chini ya barabara ambazo tunajenga. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama tunaogopa Mungu, Bibilia inasema kwamba mwanamke fulani analilia watoto wake lakini hawezi kuwabembeleza maana hawapo. Analilia waliokufa. Sisi tunatengeneza barabara na wananchi wanakaa nje. Tunajenga nyumba kubwa na kuziita nyumba za Serikali. Tunatengeneza hata Bunge letu liwe nzuri lakini wanaotutuma hapa wana kilio na wanasikitika kutoka asubuhi mpaka jioni. Ninaomba Waziri wa Wizara ya Mipango Maalum aangalie zile pesa ambazo nilisema zilirudishwa, tumpatie afidie wananchi wetu ili waweze kuishi vizuri na wawe na maisha kama ya wenzetu. Kwa hayo mengi sana, ninaomba kuunga mkono Hoja hii."
}