GET /api/v0.1/hansard/entries/305948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 305948,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/305948/?format=api",
    "text_counter": 34,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Musila",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 94,
        "legal_name": "David Musila",
        "slug": "david-musila"
    },
    "content": "Bw. Spika, itakumbukwa kwamba Swali hili lilikuja Jumanne na nikaomba ruhusa nisijibu kwa sababu sikuridhika na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa. Kwa hivyo, ningependa kumhakikishia mhe Leshoomo na Bunge hili kwamba siwezi kujibu tu kwa sababu nimeliletewa jibu. Hii ndio sababu nilikataa kujibu siku ya Jumanne; sikukubaliana na yale ambayo yalikuwa yameandikwa. Hili ni jambo ambalo tumelizungumzia kikamilifu katika Wizara. Hii ndio sababu nilisema kwamba mwaka jana nilijibu swali ambalo lilikuwa na maelezo kama haya. Kwa hivyo, tumesema sasa hatua ichukuliwe. Niko na barua hapa ya kuonyesha kwamba tumechukua hatua kamilifu tukiwa na Kamishina wa Polisi. Kutoka leo, mambo haya yako kwa Director of Public Prosecution (DPP) na Commissioner of Police. Kwa hivyo, sisi tumepeana mambo haya ili sheria ichukue mlengo wake."
}