GET /api/v0.1/hansard/entries/306532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 306532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/306532/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kingi",
    "speaker_title": "The Minister for Fisheries Development",
    "speaker": {
        "id": 27,
        "legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
        "slug": "amason-kingi"
    },
    "content": " Asante sana Bwana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangie mjadala huu. Mwanzo kabisa, ningependa kusema kwamba ninaunga mkono Hoja hii na ningependa kusema kwamba wale Wakenya ambao wameodhoreshwa katika Kamisheni hii ya kuangalia Mambo ya Mashamba ni Wakenya na watu ambao wanaweza. Ukimuangalia Mwenyekiti wa Kamisheni hii, Dr. Swazuri, utakuta kwamba ni mtu ambaye ninamjua vizuri sana. Ni mtu mchapa kazi na pia kutokana na elimu yake, ni mtu ambaye ana ujuzi sana katika mambo ya mashamba kwa sababu shahada yake ni ya Land Economics. Kwa hivyo, ni mtu ambaye kusema kweli, ataweza kuiendesha Kamisheni hii na kutupatia majibu ambayo, bila shaka, yataboresha usimamizi wa mashamba katika nchi yetu ya Kenya. Tulihitaji Kamisheni hii tangu jadi. Ni Kamisheni ambayo imechukua muda lakini angalao, Washwahili husema kwamba kawia lakini ufike. Tumechelewa kuunda Kamisheni hii lakini angalao, sasa tunaona kwamba tuko katika ile hatua ya mwisho ya kuhakikisha kwamba Kamisheni hii imebuniwa na kuanza kazi. Majukumu ya Kamisheni hii ni mazito. Kamisheni hii itahitaji kulindwa sana na Wakenya wote. Kama tujuavyo, kati ya yale majukumu ambayo Kamisheni hii itakuwa nayo, kwanza, ni kufanya uchunguzi wa hati zote za kumiliki mashamba na hati ambazo zitapatikana kwamba zilipeanwa kimakosa ama kinyume cha sheria, bila shaka, zitatupiliwa mbali. Kama ujuavyo, hakuna maskini atakayenyakua ardhi. Wanyakuzi wa ardhi ni wenye nazo au mabwenyenye wa nchi yetu. Kamisheni hii itahitajika kupambana na watu walioiba au kunyakua ardhi bila kuzingatia sheria. Hawa ndio watu Kamisheni hii itapigana vita nao. Kwa hivyo, ni kibarua kikubwa na inatubidi kama Wakenya tuwe nyuma yao kuona kwamba wamepigana na mabwenyenye hawa. Hii ni kwa sababu ikiwa bwenyenye aliiba ama alinyakua ardhi, bila shaka itakuwa si rahisi kwa mtu kama yule kukaa tu, kuangalia kwamba cheti chake kinafutiliwa mbali na Tume hii. Kwa hivyo, itakuwa ni kibarua kigumu na bila shaka sisi kama Wakenya, kuna umuhimu sana tuwe nyuma yao. Kama tujuavyo, hata wakati wa tetezi na machafuko ya baada ya kura ya mwaka wa 2007---"
}