GET /api/v0.1/hansard/entries/306534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 306534,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/306534/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Minister for Fisheries Development",
"speaker": {
"id": 27,
"legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
"slug": "amason-kingi"
},
"content": " Tunajua wazi kwamba mambo ya ardhi ilichangia pakubwa sana katika kuleta mtafaruku baada ya kura za mwaka wa 2007. Kwa hivyo, Tume hii itakuwa na fursa nzuri kuhakikisha kwamba shida ya ardhi imezikwa katika kaburi la sahau. Kama wahenga wanavyonena: “Mwamba ngoma huvutia kwake.” Ni matumaini yangu kuwa kwa sababu mwenyekiti wa Tume hii ni kijana kutoka Pwani, atafanya lolote lile kuhakikisha shida za ardhi katika mkoa huo zimetatuliwa. Kijana huyu anajua uchungu wa ukosefu wa ardhi kwa sababu ni mzaliwa wa Pwani."
}