GET /api/v0.1/hansard/entries/306563/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 306563,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/306563/?format=api",
    "text_counter": 329,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Mswada kuhusu Tume ya Kitaifa ya Ardhi, pamoja na wale Wakenya ambao wamepewa fursa ya kuhudumu katika Tume hii. Ningependa kuunga mkono yale yaliyosemwa na ndugu yangu, mhe. Mungatana. Ninajua watu wengi wanasema kwamba Tume hii ni ya Kenya nzima lakini, kama Wapwani, ni lazima tujivunie kwamba, kwa mara ya kwanza kuanzia wakati tume za kikatiba zilianza kubuniwa humu nchini, tumeweza kupata Mwenyekiti. Hatuoni aibu kujivunia kwa kupata fursa hiyo. Bw. Naibu Spika, umiliki wa ardhi nchini Kenya ni suala gumu, lakini sisi sote tunakubaliana kwamba suala hili limekita mizizi katika eneo la Pwani. Tunatumai kwamba, kupitia uongozi wa Mwenyekiti, pamoja na Makamishna wengine watakaoteuliwa kuhudumu kwenye Tume hii, suala hili, ambalo limekuwa sugu katika sehemu ya Pwani, litatatuliwa. Sote katika Bunge hili, tunafahamu kwamba suala hili limechangia kuibuka kwa makundi mbali mbali nchini, ambayo yamejaribu kupigania haki za jamii zao. Tunatumai"
}