GET /api/v0.1/hansard/entries/306565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 306565,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/306565/?format=api",
    "text_counter": 331,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kwamba Tume hii itasaidia kupunguza uhasama ambao umekuwa ukiendelezwa na makundi kama Mombasa Republic Council (MRC), wanaharakati wa kundi hilo wakijua kwamba sasa wanaweza kupata haki yao ya kumiliki ardhi. Bw. Naibu Spika, jambo la muhimu zaidi linalopaswa kuangaziwa na Tume hii ni kwamba kuna mabwenyenye wengi ambao walitumia afisi zao kunyakua ardhi katika sehemu tofauti humu nchini. Dhulma kubwa iliyotendewa Wapwani, ambayo ni miongoni mwa dhulma za kihistoria, ni kwamba ardhi kubwa katika mkoa huo haikuchukuliwa na Wakenya, bali ilichukuliwa na watu kutoka nchi za kigeni. Hili ni suala ambalo linatusikitisha zaidi. Kwa hivyo, ninatumai kwamba Tume hii itachukua fursa hii na kurekebisha hali hiyo. Kama Tume hii itawaondoa mabwenyenye kutoka nchi za nje walionyakua ardhi Mkoani Pwani, asli mia 30 ya shida za ardhi katika mkoa huo zitakuwa zimetatuliwa; kabla ya kutatua matatizo yaliyosabishwa na mabwenyenye wengine wa humu nchini. Bw. Naibu Spika, ningependa kuchukua fursa hii kuitakia Tume kila la heri. Ninajua kwamba Tume hii itakuwa na kazi ngumu. Kwa hayo machache, ninaunga mkono kubuniwa kwa Tume hii, pamoja na Makamishna waliopendekezwa, ambao majina yao tayari yameshaletwa Bunge."
}