GET /api/v0.1/hansard/entries/314919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 314919,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/314919/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Nguyai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 113,
"legal_name": "Lewis Nganga Nguyai",
"slug": "lewis-nguyai"
},
"content": "Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir. Kwanza, ningetaka kumweleza Mheshimiwa Leshomo kwamba tulituma timu kwa sababu hizo soko zilikuwa 211. Tuligawanya timu nne na tukaenda tukakagua kila soko halafu tukaanza orodha ya kuhakikisha kila soko imeisha. Ningetaka kumuhakikishia kwamba asilimia 50 zimekamilishwa. Zile ambazo ziko kwa mpangilio na ziko karibu kukamilishwa ni asilimia 23. Zile ambazo zinangojea na ziko katikati ni soko 44 na najua malalamiko mengi yametoka kwa sababu ya hizo 44 na zile 8 ambazo hazijaanza Mvita ikiwa mojawapo. Kwa hivyo, hii soko ya Mathira imeisha. Ni mpangilio wa kuifungua hatujaanza lakini tutahakikisha itafunguliwa. Ningeuliza Mheshimwa ni lini anataka tuje tuifungue. Wikendi hii, nimealikwa upande wa Elgeyo Marakwet. Naenda kwa Mheshimiwa Lina Chebii na kwa Mheshimiwa Boaz Keino na kule kwingine tutaalikwa tutahakikisha kama mimi mwenyewe siwezi kuenda kufungua, tutapata maofisa wa kuzifungua lakini kile ningetaka kusema ni ya kwamba, na sasa najibu Mheshimiwa Mwau, tutahakikisha na tumeanza orodha hiyo na mimi mwenyewe ndio naiangalia. Najua kuna Waziri ambaye amesimamia Wizara hiyo. Kila mtu ambaye soko yake haijakamilika anione mimi binafsi na nitahakikisha kwamba nitaleta mkurugenzi wa soko na tutamuambia mpangilio na hizo soko tutamaliza. Si mnipigie makofi tafadhali?"
}