GET /api/v0.1/hansard/entries/315069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 315069,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/315069/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa nafasi hii ya kuchangia katika Mswada huu ambao umeletwa na Mheshimiwa Khalwale tukijua kwamba, kwa kweli, umefika katika wakati unaofaa. Ninamshukuru Dkt. Khalwale kwa sababu mijadala yake yote katika Bunge hili imekuwa ikihakikisha kwamba taifa nzima na hasa mwananchi wa kawaida amelindwa. Ni vyema tukubali kwa kauli moja kwamba Kenya ni nchi yenye vituko. Ni nchi ambayo sarakasi zake hasa katika mambo ya hela haziishi. Nikimsikiza ndugu yangu Dkt. Khalwale, ninajihisi kwamba labda tuna nchi ambayo haina sheria ama tuna nchi ambayo ina viwango viwili vya watu. Kiwango cha kwanza ni cha watu wa juu sana na wanaoweza kufanya wanayotaka na kutembea bila kuguswa na mtu. Kiwango cha pili ni"
}