GET /api/v0.1/hansard/entries/315071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 315071,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/315071/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "cha watu ambao wanastahili kunyanyaswa tangu utoto wao hadi watakapoondoka kuatika taifa hili na kuenda zao. Tukiangalia nyuma, tunaona wizi wa hela ambao umetokea katika taifa letu. Ni juzi tu tulikuwa na kizaazaa cha mambo ya mahindi katika Bunge hili. Hadi leo, huo wizi haujatatuliwa na mambo hayo yamewekwa yamekaliwa. Watu wanatembea wakiona kwamba wale walionyanyaswa wanateseka. Pesa za Triton, ni juzi tu zilizungumziwa. Mabilioni ya pesa yalinyakuliwa na watu na hadi leo, kumekuwa ni kisanga cha vuta nikuvute si hapa wala pale. Kunapozungumzwa, unasikia mwizi aliyeiba yuko nchi fulani. Waliohusika na unyakuzi wa mali ya umma wako hapa nchini na hakuna chochote kimetokea. Leo, tunaongea mambo ya De la Rue. Ni matarajio yangu kwamba tutayazungumuza mambo haya leo, tufike kikomo chake na kuona kwamba mchezo umeisha. Hakuna mtu ana uwezo au uhuru wa kuingia na kuharibu mali ya wananchi wa Kenya na kutembea anavyotaka. Katika wizi kupitia kwa pyramid schemes mwaka nenda, mwaka rudi, tumekaa hapa na kutoa hela za kufanya kazi hasa kwa kitengo cha NSIS. Idara hii imepewa pesa na Bunge kila mwaka. Idara ya CID imepata pesa hapa kupitia Kamishena wa Polisi wa taifa letu. Hela tulizotoa zifanye kazi katika NSIS, ambayo kazi yake ni kuangalia mambo kama haya na kutoa taarifa mahali inatakiwa na hatua kuchukuliwa, hazikufanya hivyo. Ni kwa nini pyramid schemes zilianzishwa na pesa nyingi za wananchi zikapotea? Pesa zilizotajwa hapa na Mheshimiwa Khalwale zinafahamika zilipo. Tumeongea mambo haya hapa katika Bunge hili hata kabla ya kuhama na kuenda Bunge la Zamani. Vile vile, tuliongea mambo haya kule. Je, tuna Serikali na watu walio na masikio ambao wanasikia wananchi wanavyosema ama hili limekuwa jambo la mzaha tu kuanzia mwaka wa 1963 tuliponyakuwa Uhuru wetu? Waliokuwa mbele yetu, marehemu Paul Ngei, Masinde Muliro na wengine wamekaa hapa na kuzungumza. Ni hatua gani imechukuliwa hata siku moja? Kwangu, kuna watu waliopoteza pesa. Wengine ndoa zimevunjika. Mpaka leo, zinaendelea kuvunjika kwa sababu umaskini ukiingia katika nyumba ambayo bibi na bwana walikuwa wakifanya kazi, na bibi ndiye aliamua kuchukua hela na kuweka katika miradi hii ya uwongo, kunakuwa na ugomvi na ndoa zinavunjika. Kuna watoto waligombana na baba zao. Leo, tumedhihirishiwa hapa kwamba wezi walioiba pesa hizi, wanajulikana. Mheshimiwa Boni Khalwale amewataja. Hata Kampuni zao amezitaja na sehemu zinazomilikiwa na wezi hao. Je, wananchi wa Kenya wanatakiwa kufanya nini? Mwizi anajulikana, pesa alizoiba zinajulikana ziko katika benki; zingine zilitumika kununua viwanja na zingine kununua ploti. Zingine zimetumika kwa kujenga. Ukienda katika jela, utapata limejaa wezi wa kuiba kuku, mbuzi na kondoo lakini wezi wanaoiba hela kama zile zinazotajwa hapa ni kama wao ndio mawakili, majaji na maofisa wanaoweka watu katika jela. Mimi ninazungumuza kwa uchungu sana kwa sababu sioni ni kwa nini nchi ambayo ina Rais, makamu wake na Waziri Mkuu, Mawaziri na Kamishena wa Polisi, tunaongea mambo haya hapa. Tungekuwa tunaongea mambo ya kuendeleza nchi hii mbele. Lakini tuko hapa kudai haki ya mwananchi ambayo “imeibiwa”. Hivi sasa, tunaongea kuhusu migomo ya walimu na madaktari. Walimu wengi waliweka pesa zao katika miradi hii. Wengi waliozichukua wako katika Bunge hili. Mheshimiwa Khalwale amesema ni uongozi wa juu uliohusika kuwaibia wananchi. Kwa"
}