GET /api/v0.1/hansard/entries/315073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 315073,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/315073/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hivyo, kama sio uongozi wa juu, hatua ingekuwa imechukuliwa. Ni hao walimu ambao baada ya kupoteza pesa, tunafanya mikataba na wao na kuwaahidi kwamba pesa zao zitalipwa. Waziri wa Elimu anatengeneza mkataba na walimu kwamba watalipwa pesa zao na mwaka unapita na hawapati pesa zao. Pyramid schemes zinanyakua ile kidogo wako nayo na hapa, mabepari wengine wanachukua pesa nyingi na kukataa kuwalipa. Hao ndio watu tunategemea wasomeshe watoto wetu. Madaktari nao wanaagiziwa nyongesa ya mshahara baada ya miaka miwili. Wakati huo ukifika, maneno yanabadilika inakuwa hakuna pesa za kuwalipa. Mimi ninasema hivi kama mtu aliyechaguliwa na wananchi wa Kenya kuwawakilisha, kupitia eneo la uwakilishi Bunge la Kangundo, kwamba tuupitishe Mswada huu mara moja naye Rais autia kidole ili kazi ifanyike. Sisi hatutaki kuona Mhe. Rais anatia kidole Miswada ambayo inafaidi Serikali peke yake. Hatutaki kuona ile ya mwananchi kama hii, inafika kwake na inakaa miezi kumi. Tutafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba kidole kimetiwa na hatua imechukuliwa. Kama Serikali haifanyi kazi, basi tunataka tuambiwe tufanye nini na tuende wapi. Kama Serikali haifanyi kazi haina haja kuwa mamlakani. Kama kazi imewashinda, tumeunda sheria na haiwezi kutumika na mwananchi kupewa haki yake, sioni kuna haja gani kusema tuko katika Bunge la Kumi, na tunaelekea kumaliza muhula wetu na hali hili Bunge likipitisha jambo fulani, halifanyiki. Wakenya wanaendelea kuchoka na uamuzi wa Wakenya baada ya kuchoka hautakuwa uamuzi wa amani. Utakuwa uamuzi wa matatizo makubwa sana. Matatizo yakiingia, mabepari ndio watu wa kwanza kuumia. Wajue kwamba wakikaa katika nyumba kubwa na kuendesha magari makubwa, mwananchi wa Kenya atakapochoka atatumia mbinu zozote kujiokoa. Hii ni hata kama itabidi alale barabarani akanyagwe na gari, itakuwa hivyo. Jambo hili likitokea bepari atakuwa na maiti ambazo hawezi kuzika katika taifa hili kwa sababu zitakuwa nyingi sana. Harufu ya maiti itaharibu nchi. Hili si jambo la mchezo. Ninataka kusema kwamba ninaunga mkono Mswada huu na moyo wangu wote na nguvu zangu zote na kusema kwamba tuupitishe ili Wakenya wasaidiwe. Kwa hayo, niaunga mkono."
}