GET /api/v0.1/hansard/entries/315711/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 315711,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/315711/?format=api",
"text_counter": 544,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, Waislamu tumeonyesha kwamba hakuna fikra ya vita baina ya dini ya Kiislamu na dini ya Wakristo kama yale yaliotokea Garissa. Ni Waislamu waliokwenda kwenye Kanisa siku ya Jumapili na wakayalinda makanisa yale. Ninapenda kuwafahamisha wenzangu hapa kwamba wale waliofanya vitendo hivyo, baadhi yao walikwenda kwenye vilabu vya pombe maarufu kama bar na wakaiba chupa za pombe. Hakuna Mwislamu ambaye atakwenda kuiba chupa za pombe kwa sababu ya huzuni ya kifo cha Marehemu Sheikh Aboud Rogo. Haya yote hayajafanywa na wafuasi wa Aboud Rogo bali na watu ambao wanataka kuleta chuki baina ya Waislamu na Wakristo nchini. Ni lazima sisi sote viongozi wa dini tufanye kazi pamoja kuangamiza hila za watu wanaotaka kuleta uhasama na chuki baina ya wafuasi wetu. Lengo lao kuu ni kuharibu amani na umoja wa wananchi wote hapa nchini."
}