GET /api/v0.1/hansard/entries/315713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 315713,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/315713/?format=api",
"text_counter": 546,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tunataka Serikali ifanye uchunguzi wa kina na haraka ili tujue ni akina nani waliomuua Sheikh Aboud Rogo. Ni lazima wachukuliwe hatua kuambatana na sheria za nchi hii. Kufikia sasa tungependa kujua ni watu wangapi wameshikwa kuhusiana na kifo hiki cha kinyama kilichotokea mchana barabarani kuu ya Bamburi. Sheikh Aboud Rogo alipigwa risasi 22 mbele ya mke wake, mwanawe wa kike wa umri wa miaka saba na mbele ya baba ya mke wake. Haya yote yalitokea mchana na tunaweza kuyalinganisha na maafa yaliyotokea Wilaya ya Tana River mchana saa kumi na mbili wiki iliyopita ambapo watu 52 walipoteza maisha yao. Ni huzuni kuwa kufikia sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na maafa haya."
}