GET /api/v0.1/hansard/entries/317071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 317071,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/317071/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mrs. Leshomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Madam Naibu Spika wa Muda, ningependa kumshukuru Waziri kwa ile kazi nzuri anayoifanya. Ningependa waangilie ambulances na pikipiki ambazo walitoa. Waunde sheria kwa sababu hizo pikipiki na ambulances sio matatu. Kama mtu ni mgonjwa, unaambiwa uweke mafuta ili waende kuchukua mgonjwa. Ningependa kumwambia Waziri aunde sheria ya kulinda hizo ambulances na pikipiki. Watu wetu hutegemea mifugo. Wanauza mifugo ili pengine wapate pesa ya kupeleka mgonjwa hospitali. Kama mtu ni mgonjwa usiku, utaenda kuuza mifugo saa ngapi ili uweke mafuta kwa gari? Naomba Waziri atusaidie kwa sababu tuna shida kubwa."
}