GET /api/v0.1/hansard/entries/317182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 317182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/317182/?format=api",
"text_counter": 372,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bi Naibu Spika wa Muda, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Ningetaka kumshukuru mhe. Chachu kwa kuuleta Mswada huu katika Bunge ili tuweze kuuchangia. Taifa la Kenya ndilo taifa la kipekee ambapo uongozi wa juu unaruhusiwa kufanya unavyotaka na kutoa mateso bila chuki kwa Wakenya. Hatungekuwa tunaongea kuhusu ukame katika taifa letu kama tungekuwa tunaliongoza vilivyo na kuangalia mbele ili kuona linaelekea wapi. Tutaunda jopo hili halafu tuunde lingine na lingine. Umekuwa ni mwito kwa Wakenya kuendeleza sera za aina hii. Uongozi wetu ulikuwa ni wa kuunda tume na mambo mengine lakini mwishoni hakuna kinachotokea. Katika nchi hii tuna maji. Tuna mito miwili ambayo inajaza maji katika bahari letu la Hindi. Maji ya mto Tana yanapita bila kutumiwa na kuguswa na mtu. Maji ya mto Athi yanaelekea baharini bila kutumiwa na kuguswa na mtu. Hivi leo, mto huo umegeuzwa kuwa mtaro wa kusafirisha uchafu unaotoka Nairobi, Athi River na Thika. Maji yanayoingia Bahari Hindi huwa yamejaa uchafu. Ikiwa Wizara ya Maji ingefanya kazi inavyostahili tusingekuwa na shida ya maji nchini mwetu. Sisi tunataka tu kupigana na njaa na ukame lakini maji yanaachwa. Tunalia kwamba kuna ukame katika taifa letu. Maji ya Ziwa Victoria yanawalea na kuwalisha Wamisri kule kwao. Maji haya yanatoka huku kwetu bila kutumika ilhali tunalalamika kuna ukame. Ingekuwa tunajitoa mhanga kuangalia maslahi ya wananchi, taifa letu lisingekuwa na shida hata kidogo ya ukame. Kwa hivyo, uongozi wa juu na wenye kupanga mipango kuhusu jinsi maji yatakavyotumika katika taifa watoke kwenye maofisi zao. Waache kupanga mambo ya kujipatia magari makubwa ya kutembea nayo, kujilipa marupurupu ya kutumia wakiwa safarini na kufanya safari zisizofaa. Inawapasa wafike mashinani kufanya kazi. Wasipofanya hivyo, tutakuwa na taabu katika taifa letu. Naomba kwa unyenyekevu kwamba waliopewa madaraka ya kufanya kazi waache mipango ya kupotosha watu. Waache kusema,”Mimi ni mkurugenzi wa shirika hili.” Waingie kufanya kazi. Mhe. Shebesh amesema jambo ambalo lapaswa kuangaliwa. Tunapatwa na njaa huku kwetu. Watu wanakufa na inatubidi kutumia hela zinazoweza kuweka maji hapa kununua chakula nje ilhali ukienda pale Kinangop utaona viazi vikiozea barabarani kwa vile havina mwenyewe. Makabeji vile vile. Bi. Naibu Spika wa Muda, mahindi ya hapa Kenya utagundua kwamba yanaoza na hali wakulima hawajalipwa pesa zinazowafaa huku tukisema kwamba kuna njaa. Ikiwa tutapanga mipango sawa ya kujimudu, taifa letu litasimama imara na hatutakuwa na ukame. Isitoshe, pasingekuwepo na ukosefu wa kazi kwa sababu vijana wetu wanaofurika mijini wanafanya hivyo kwa sababu hakuna ajira kule wanakotoka. Tumeweka pesa mijini. Tunazunguka nazo mijini. Tunazitumia huko mijini. Tunajiwekea mishahara mikubwa. Maandamano ya walimu na madaktari ni kwa sababu ya usimamizi mbaya wa uchumi wa taifa letu. Naunga mkono. Watakaoingia kwenye halmashauri hii wafanye kazi vizuri kwa kuwa watakuwa wanatumikia taifa hili."
}