GET /api/v0.1/hansard/entries/317214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 317214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/317214/?format=api",
    "text_counter": 404,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Yakub",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 378,
        "legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
        "slug": "sheikh-dor"
    },
    "content": "inatuahidi mara kwa mara ndani ya Bunge – na kufanya mito hiyo iweze kubadilishwa na kutumiwa kwa mipangilio ya unyunyizaji maji. Lakini ni masikitiko kwamba mpaka sasa, Serikali haijakuwa na moyo wa kuweza kuondoa maswala ya ukame. Madam Spika wa Muda, ukame huja kwa njia mbili na moja ni kupitia kwa binadamu mwenyewe. Ninaamini kwamba utawala wa nchi yetu umechangia kwa maswala ya kuleta ukame. Tunatarajia kwamba taasisi ambayo itapitishwa itakuwa moja ambayo itaweza kuondoa njaa na ukame, na haswa katika maeneo ambayo mito hiyo inapitia. Kama nilivyotaja, Mto Tana una umbali wa kilomita 1,000 au maili 620 lakini hakuna jambo lolote linalofanywa. Mwisho, maji ya mto Tana yanaishia Bahari Hindi. Hili ni jambo ambalo tunataraji taasisi hii ikiwekwa pahali pake sawa sawa, kama ilivyoelezwa na Bw. Chachu, itaweza kuondoa shida ya ukame."
}