GET /api/v0.1/hansard/entries/317652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 317652,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/317652/?format=api",
"text_counter": 422,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children, and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Bi. Naibu Spika wa Muda, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuzungumzia suala hili la uchaguzi. Marekebisho haya yanakuja katika muda sawa wa kurekebisha zile sheria ambazo tulikuwa tumepitisha. Hata hivyo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ina jukumu kubwa sana kututoa katika sifa mbaya tuliyokuwa nayo kutoka 2007 hadi mwanzo wa 2008. Janga hilo lililopata Kenya lilikuwa kubwa sana. Tukumbuke kwamba siyo jukumu lao peke yao kufanya kazi hii ikiwa sisi pia hatutaweza kuwapatia uwezo na vile vile kufanya kazi nao. Tume hii Huru ya Uchaguzi na Mipaka ina jukumu kubwa sana. Zaidi hayo, inawapasa wakumbuke kwamba maisha ya Wakenya yanawategemea wao. Usalama katika uchaguzi unaokuja utategemea vile kazi itakavyofanywa kwa haki na uwazi. Tume hii Huru yaUchaguzi na Mipaka sharti ikumbuke kwamba wao si tume ya biashara ya kutengeneza hela. Hawakwenda pale kutengeneza hela ila wako pale kuwafanyia Wakenya kazi kwa kuwapatia uchaguzi unaofaa na tena wa haki."
}