GET /api/v0.1/hansard/entries/318234/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 318234,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/318234/?format=api",
"text_counter": 386,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na kaka yetu wa Benki Kuu ya Kenya (CBK), wameachishwa nyadhifa zao. Inasemekana walitoka nje wakapeana fedha. Katika miaka yangu yote nimefanya kazi ya uhasibu mambo ya rushwa sihusiani nayo. Ukweli ni kwamba kuna Wabunge wengi hapa ambao hawahusiki na mambo ya rushwa. Kwa hivyo, kuwekwa katika kapu moja la kundi la wapokeaji rushwa ni jambo linaloshusha hadhi ya Bunge, hadhi yako, hadhi ya Wabunge, na mimi kama Mbunge wa Wundanyi ni jambo linaloshusha hadhi ya watu wangu ambao ninawawakilisha. Kwa hivyo, naomba ulichukulie jambo hili kwa mzigo. Ulichukulie hatua zinazofaa ili tupate kusafishwa maana hata ukienda mjini utasikia, “unawaona wale wachukuwa-rushwa?” Ukipeleka gari unaambiwa unaweka petroli na pesa za rushwa. Bw. Spika tunaomba kwa hisani na heshima yako ukomboe hili Bunge katika hii hali imejikuta. Naomba uchukuwe ombi letu na uliweke maanani."
}