GET /api/v0.1/hansard/entries/320340/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 320340,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/320340/?format=api",
    "text_counter": 306,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, Waziri ameelezea mikakati ya Serikali kuhusu barabara hizi. Barabara zinazoangaziwa hapa, ambazo zimefanyiwa makadirio ya gharama za ujenzi, ziko katika sehemu za wafugaji. Tunakumbuka wakati fulani Rais Kibaki alitembelea eneo hilo na kutoa ahadi kuhusu barabara hizo, lakini hakutimiza ahadi hiyo. Waziri Mkuu pia alitembelea eneo hilo hivi majuzi na kutoa ahadi kama ile ya Rais, lakini hajatimiza ahadi hiyo. Alipokuwa akizindua rasmi shughuli ya ukarabati wa barabara kule Kitale, Rais Kibaki alitoa ahadi lakini mpaka sasa ahadi hiyo haijatimizwa. Je, ni mikakati gani ambayo Waziri ameweka kuhakikisha kwamba viongozi hao vigogo hawataendelea kuwahadaa wananchi kwa kuitisha mikutano ya uzunduzi rasmi wa shughuli za ujenzi wa barabara na baadaye kutokomea, wasionekane tena mpaka baada ya uchaguzi?"
}