GET /api/v0.1/hansard/entries/32040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 32040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/32040/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Joho",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 30,
"legal_name": "Hassan Ali Joho",
"slug": "hassan-joho"
},
"content": "Waziri Msaidizi, sijui kama umewahi kupata nafasi ya kutembea Mombasa hivi karibuni. Ikiwa imepita kwenye Daraja la Nyali, utakubaliana na mimi kwamba mtu anachukua zaidi ya masaa manne kuvuka daraja hilo lenye urefu wa kama mita 100 hivi, kwa sababu ya magari mengi na binadamu wengi wanaotumia daraja hilo. Sisi tunajua kwamba upande wa Nyali wa daraja umeangukia jengo la Tamarin Village, na upande wa mjini wa daraja umeangukia nyumba ya kibinafsi. Utachukua hatua gani, kwanza, kwa sababu ya usalama wa watu wanaoishi upande wa Nyali, kurudisha mali ya umma kwa Serikali? Pili, utachukua hatua gani kuhakisha kwamba tuna mipango kabambe ya kujenga daraja mpya mahali ilipokuwa daraja ya zamani?"
}