GET /api/v0.1/hansard/entries/32041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 32041,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/32041/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kinyanjui",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 48,
        "legal_name": "Lee Maiyani Kinyanjui",
        "slug": "lee-kinyanjui"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, ningetana kukubaliana na mheshimiwa. Kama alivyosema, msongamo wa magari, haswa katika sehemu ya Nyali, umezidi kiwango. Hata hivyo, nilisema hapo awali kwamba Wizara, kupitia halmashauri ya KURA, imetangaza mpango wa kujenga daraja ya pili, ambayo itaunganisha sehemu ya kisiwani na bara ya mji wa Mombasa. Hata hivyo, ningependa kumhakikishia mhe Joho kwamba tumetoa ombi letu kwa Wizara ya Ardhi ihakikishe kwamba ile ardhi ambayo imenyakuliwa na watu binafsi, vikiwemo vile vipande nilivyovitajwa na vinginevyo, imerudishwa kwa umma ili tuweze kujenga hilo daraja ya pili, na tuweze kupunguza msongamano wa watu na magari."
}