GET /api/v0.1/hansard/entries/32048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 32048,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/32048/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. Nimemnukuu Waziri Msaidizi akinena kwamba wao, kama Wizara, wanatambua kwamba vipande vya ardhi ambavyo vilikuwa vya Serikali vilinyakuliwa na sasa wanapanga kuvirudisha kwenye milki ya Serikali. Ninatarajia atueleze mikakati kabambe. Ni hatua gani ambayo tayari wamechukua, kama Wizara, na wamefika wapi, ili kuirudisha ardhi hiyo kwenye milki ya Serikali ndio barabara ipanuliwe?"
}