GET /api/v0.1/hansard/entries/320494/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 320494,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/320494/?format=api",
    "text_counter": 460,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaomba nitoe mchango wangu kwa Mswada huu ili ibainike wazi wazi kuwa Waziri amejaribu awezavyo kuleta mabadiliko katika idara hii ambayo inahusika na usafiri. Kitu cha kwanza ningeomba Waziri atie maanani ni kuwa tumepatwa na maafa mengi sana barabarani na kuwa nia haswa ya Mswada huu ni kuhakikisha kuwa maisha ya binadamu yanaangaliwa vilivyo. Kwa hivyo, itakuwa ni jambo ambalo litatufaa tukiangalia hivi vipengele vyote ambavyo vinajaribu kulegeza sheria ili uendeshaji wa magari njiani uwe unakosa nidhamu. Kitu cha kwanza, sijaona popote katika Mswada huu ambapo Waziri ameangalia kwa uangalifu utumiaji wa rununu wakati mtu anapopeleka gari. Kwa wale ambao labda hawajaelewa sawa sawa, ninamaanisha wale watu ambao wanatumia simu za mkononi wakati wanaendesha magari. Naomba Waziri aangalie kuwa hawa watu wameadhibiwa vikali kwa sababu huwezi kutumikia mabwana wawili. Aidha unapeleka gari ama unasikiza simu. Mara nyingi tumeona ajali zimetokea kwa sababu ya watu wanaozungumza kwa simu baadala ya kushughulikia mambo ya kuendesha gari. Bw. Naibu Spika wa Muda, nilifadhaika kumsikia mwenzangu akitoa maoni yake kuhusu Mswada huu, kuhusu uendeshaji wa gari ukiwa mlevi. Ninamshukuru Bi Odhiambo-Mabona, kwa matamshi yake ya kusema sheria lazima izingatiwe. Huwezi kutoka pahali ulipokuwa huku ukiwa mlevi na unaingia ndani ya gari na unajua wazi wazi kuwa unaenda kusababisha vifo vya wengine. Ukienda kwa mahospitali hivi sasa, utapata watu wengi wamelazwa, miguu imepandishwa juu kwa sababu ya ajali za barabarani. Nyingi za ajali hizi zinatokana na"
}