GET /api/v0.1/hansard/entries/320496/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 320496,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/320496/?format=api",
"text_counter": 462,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "uendeshaji mbaya, hasa mara nyingi watu wakiwa walevi. Ni ombi langu kwa Waziri ahakikishe kuwa adhabu kali inatolewa kwa watu ama mtu yeyote anayepeleka gari akiwa amelewa. Vile vile, ninamwomba Waziri aiangalie sheria hii ili tuhakikishe kwamba madereva wa magari ya abiria hawayaendeshi magari hayo kwa kasi zaidi ya kile kiwango ambacho kimeruhusiwa na sheria. Mara nyingi, tunakutana na magari ya abiria kutoka Nairobi yakielekea Mombasa. Licha ya kwamba uko na gari ndogo, unaona magari hayo yakikupita kana kwamba umesimama barabarani. Magari hayo huendeshwa kwa kasi zaidi. Yanapokutana ya mnyama ama mtoto akivuka barabara, mara nyingi ajali hutokea. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine la kusikitisha ni kwamba, chini ya Kipengele 36, Waziri amependekeza kwamba mtu atakayepatikana akiendesha gari bila ya leseni ya kuendesha gari apigwe faini ya Kshs100. Ninamwomba Waziri ayatilie maanani mambo haya. Kwa nini mtu apigwe faini ya Kshs100? Kama ni hivyo, basi haina haja ya kumpiga mtu faini kwa kosa hilo. Ni lazima tuweke faini ambazo zitawafanya watu kuogopa kuvunja sheria. Mara nyingi, watu huvunja sheria wakijua kwamba watakaposhikwa na polisi na kushtakiwa, watapigwa faini ya Kshs100 ama Kshs1,000. Mtu kama huyo atalipa faini na kuendelea na mambo yake."
}