GET /api/v0.1/hansard/entries/320498/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 320498,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/320498/?format=api",
"text_counter": 464,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninamwomba Waziri anisikize, kwa sababu ninaona anajishughulisha na “mjadala” mwingine. Namwomba anisikize kwa sababu yeye pia hutumia barabara ya kwenda Mombasa mara kwa mara, na huenda akapatwa na adhabu kama hii. Ni lazima walevi watakaopatikana wakiendesha magari waadhibiwe. Mswada huu unasema kwamba dereva asiendeshe basi kwa muda wa masaa manane kwa siku. Safari ya basi kutoka Nairobi hadi Mombasi huchukua zaidi ya masaa manane. Jee, madereva wa mabasi watabadilishwa zamu njiani ama itakuwaje? Ninamwomba Waziri afikirie kuhusu suala hilo."
}