GET /api/v0.1/hansard/entries/322743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 322743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/322743/?format=api",
"text_counter": 498,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama hapa kuunga mkono Hoja hii shingo upande. Ukiangalia orodha hii ya majina, utaona ya kwamba Bw. Murshid aliomba kuwa mwenyekiti, lakini hakupendekezwa kama mwenyekiti bali kama komishina. Je, ni kwa nini jina la Jean Kamau ambaye pia ni mwanasheria halikuteuliwa kama mojawapo wa makomishina katika orodha hii? Ni kwa nini mhe. Rais na mhe. Waziri Mkuu hawakuona haja ya kulijumuisha jina lake katika orodha hii? Haya ni makosa na maonevu kwa akina mama. Halikuwa jambo la busara kufungia nje la Jean Kamau kwa sababu yeye angefanya kazi kama wanaume ambao wamependekezwa katika orodha hii. Angalipatiwa nafasi ya kuhudumu kama komishina. Je, aliachwa nje kwa sababu gani? Haya ni baadhi ya maswali yanayonifanya niunge mkono Hoja hii shingo upande na nikiwa na roho nzito."
}