GET /api/v0.1/hansard/entries/324182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 324182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/324182/?format=api",
"text_counter": 468,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa nafasi hii. Kwanza, ningependa kumpongeza rafiki yangu kwa kuteuliwa Waziri. Natumaini kwamba ng’ombe wake sasa waitakoma kulisha kwangu. Bw. Naibu Spika wa Muda, Mswada huu umekuja wakati unaofaa. Nchi hii imeathirika mara nyingi kwa sababu ya hao wenzetu ambao huwa hawana imani ama fikira wanapotenda uhaini katika nchi yo yote ile. Mswada huu umekuja wakati tunapoitekeleza Katiba mpya. Isingekuwa hivyo, tungehofia kwamba sheria hii itakapotekelezwa kikamilifu ingeleta madhara kwa watu wengine lakini vipengele fulani vya Katiba vinahakikisha kwamba hakuna mtu yeyote ambaye ataadhirika. Wakati umewadia kwa nchi hii kuhakikisha kwamba sheria kama hizi za kutuwezesha kupambana na uhaini na uharamia zinatekelezwa kikamilifu ili kulinda maslahi ya nchi hii. Kama walivyosema wenzangu waliotangulia, ninaomba kuchangia kwa undani. Hivi majuzi, Bunge hili lenyewe lilikuwa katika hatari kubwa ya kushambuliwa na magaidi, kama tulivyoelezwa. Ninashukuru kwamba wale wanaohusika na utendaji haki na utekelezaji wa sheria walichukua hatua zinazofaa na kuhakikisha kwamba maharamia hao walipata kifungo walichostahili. Kwa hayo machache, ninauunga Mswada huu mkono."
}