GET /api/v0.1/hansard/entries/325718/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 325718,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/325718/?format=api",
"text_counter": 388,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana Mh. Naibu Spika wa Muda. Ninataka kujiunga na wenzangu kuzungumza juu ya Tume hii ya Uwiano na Mariadhano ya kitaifa ambayo imepewa muda wa kuendelea na kazi, hasa makomishna walioko. Makomishna wako na kazi kubwa ya kufanya. Makomishna hawa wanafahamu ya kwamba kazi yao ni kuleta jamii za Wakenya pamjoa bila wao kukosana ovyo ovyo na kuzozana, haswa wakati huu tuko karibu kuenda kwa uchaguzi. Ninataka kumpongeza Mheshimiwa Baiya na Kamati yake kwa kazi nzuri waliofanya, na wenzangu Wabunge ambao walizungumzia swala hili. Jambo ambalo ningependa kuwatajia makomishna hawa ni kwamba, wasisahau ya kwamba mwanasiasa yeyote anakula chakula chake. Ni kashfa kuwa wenzetu wanataka viti. Kwa hivyo, waangalie sana kuwa wasije wakatunyima kuzungumza ama kutufunga midomo ili tusiweze kuomba kura vile inavyofaa. Asante sana. Ninawapongeza kwa ile kazi waliofanya, lakini waweze kuifanya na kuimalizia kwa muda wa mwaka huu mmoja ambao wameongezewa."
}