GET /api/v0.1/hansard/entries/328826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 328826,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/328826/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bi Naibu Spika wa Muda, ninataka kumuuliza Waziri kama ana habari kwamba mabwawa mengi ya maji yaliyoweza kufanyika katika taifa letu yanachimbwa tu na kuwachiwa wananchi maji bila kuyaangalia na kujua kama yanafaa au hayafai. Maji mengi yamekuwa na chumvi na hakuna njia yote iliyoweza kuonekana ya kwamba kuna tegemeo lolote la kuweza kutatua tatizo hilo kwa kuleta madawa ya kutoa chumvi na vile vile kutoa uchafu. Wananchi wengi wamekunywa maji, meno imeharibika na afya yao zimekuwa katika hali ya kutatanisha. Waziri ana habari hiyo na kama anayo, anategemea kufanya nini kutoa taabu hiyo kwa Wakenya?"
}