GET /api/v0.1/hansard/entries/328834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 328834,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/328834/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Nuh",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 114,
        "legal_name": "Nuh Nassir Abdi",
        "slug": "nuh-abdi"
    },
    "content": "Bi Naibu Spika wa Muda, mara nyingi kama waheshimiwa Wabunge tunasema Mawaziri wengi hufika hapa Bungeni na majibu ambayo si kamilifu kwa maswali yeetu. Mfano mzuri ni jibu la Waziri huyu. Jibu hili linasema mradi huu utaanzishwa mwaka huu na utakamilika katika kipindi cha miaka miwili. Kabla ya yeye kujibu Swali hili, nilimunong’onezea kwamba akilijibu hivi itabidi aeleze Bunge ni pesa ngapi wametenga kwa mradi huu katika mwaka huu. Hii ndio maana amebadilishe jibu lake na kusema wakati huu wahandisi wanafanya michoro ya mradi huu. Ni lini Wizara hii itapata michoro hii kutoka kwa wahandisi? Michoro hii ilikamilika miaka miwili iliyopita. Mimi nina nakala ya ripoti ya wahandisi. Je, Waziri aliangalia jibu alilopewa na maafisa wake kabla ya kufika hapa Bungeni au aligundua hakuna pesa za kukamilisha mradi huu baada yangu kuuliza Swali hili? Ni pesa ngapi wametenga za mradi huu katika mwaka huu?"
}